Kamusi ya Wanafunzi

Filters
  • Kamusi ya Wanafunzi

    Kamusi ya wanafunzi ya Kiswahili – kiingereza ni kamusi inayowalenga wanafunzi wa ligha zote mbili ambao hawajapata umilisi kamili wa lugha mojawapo au ambao ndio kwanza wanaanza kujifunza Kiswahili. LLi kutimiza lengo hili, kamusi hii inayosisitiza ‘uwili lugha’ imepangwa kwa ustadi mkubwa ili kuwapa wasomaji wake msamiati wa msingi wa lugha zote mbili; ikianza na Kiswahili ambayo ndiyo lugha kuu ya mawasiliano (Lingua Franka) ya watu wa Afrika Mashariki na eneo la maziwa makuu.

     

    Mpangilio wa vidahizo, tafsiri na maelezo na mifano ya matumizi ya vidahizo katika sentensi ni nakshi inayoamsha hamu ya msomaji mara moja. Katika mpangilio huu, maelezo na msamiati wa msingi wa lugha hizi mbili, ikianza na kidahizo katika Kiswahili, kategoria ya neon, (yaani: kitenzi, kivumishi, kielezi n.k), ngeli (katika nomino), kasha kisawe cha kiingereza, mifano yanjeo, na matumizi katika sentensi yametolewa.

     

    Baadhi ya yanayodhihirisha upekee wa kamusi hii ni pamoja na:

    • Misamiati katika lugha mbili – Kiswahili na kiingereza
    • Usarufi wa maneno kupita vitengo na kategoria zake
    • Mifano ya sentensi kwa kila kidahizo
    • Mwainisho wa visawe, vitawe na vitate
    • Mifano ya methali na misemo mbalimbali
    • Picha na michoro anuwai nay a kupendeza kwa vidahizo kadha
    • Picha na michoro mbalmbali ya miti, mimea na matunda mbalimbali

     

    Kamusi hii imetungwa kwa ustadi wa hali ya juu na mwanaleksikografia mwenye utalaamu na uzoefu wa miaka mingi. Hii ni dafina kuu kwa wanafunzi wote wanaopenda kufahamu na kuwa na umillisi kamili na utendaji wa lugha ya Kiswahili.

     

    UGX 38,000
Kamusi ya Wanafunzi
Longhorn publishers' websiite uses cookies to improve your experience. By using this website you agree to our Data Protection Policy.
Read more